Download: Kyanguli Miaka Kumi Baadaye

By Kenya CitizenTV

475

TIP: Right-click and select "Save link as.." to download video

Initializing link download... Initializing link download.....

Usalama wa wanafunzi hasa katika shule za malazi kwa siku za hivi karibuni umetiliwa shaka kutokana na kuongezeka kwa mikasa ya moto ambayo kiini chake mara nyingi huwa hakibainiki wazi. Kwa hivyo usimamizi wa shule mbali mbali umeamua kutilia mkazo usalama wa wanafunzi wake hasa katika mabweni kwa kuzingatia mikakati na mbinu za ujenzi zinazowawezesha wanafunzi kukwepa moto iwapo itatokea. Basi mwanahabari wetu Anders Ihachi alizuru shule ya upili ya Kyanguli kaunti ya Machakos na anatuletea taarifa inayogusia hatua ambazo shule hiyo imepiga kama mfano mzuri, tangu kukumbwa na mkasa mbaya wa moto mwaka 2001, ambapo wanafunzi 67 waliangamia.